Ndege ya kijeshi yaanguka DR Congo
Ndege ya kijeshi imeanguka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuwaua abiria wote.
Maafisa wa maswala ya angani wamesema kuwa ndege hiyo ilifeli kupaa vizuri kutoka uwanja wa ndege wa N'djili katika mji mkuu wa Kinshasa na kuanguka katika makaazi ya Nsele.
Haijabainika iwapo kuna watu wowote waliouawa ama kujeruhiwa ardhini.
- Zaidi ya wafungwa 900 watoroka gerezani DRC
- Rais Kabila azuru nchini Tanzania
- Miili ya wataalamu wa UN yapatikana DRC
- Shambulio dhidi ya upinzani DRC
Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Kinshasa amesema kuwa ndehe hiyo ilikuwa ikibeba mizigo na kwamba haikuwa na abiria wowote.
Ripoti nyengine zinasema kuwa baadhi ya wanajeshi waliuawa.
No comments