Serikali Yatoa Onyo kwa Wafanyabiashara ya Mbolea
Wafanyabiashara wa mbolea nchini wametakiwa kuuza bidhaa hiyo kwa kufuata bei elekezi zilizotangazwa na Waziri wa Kilimo na Mifugo Dkt. Charles Tizeba , kwani lengo la serikali ni kuhakikisha wakulima wanapata mbolea ya uhakika na kwa be nafuu.
Agizo hilo limetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea TFRA Bw. Lazaro Kitandu, katika mahojiano aliyoyafanya na vyombo vya habari, kufuatia taarifa za kuwepo kwa wafanyabiashra wachache wanaotaka kuvuruga nia hiyo nzuri ya serikali kwa kuanza ulanguzi wa mbolea
Aidha, Bw. Kitandu alitaja sababu ya kuwa na bei elekezi ya mbolea kuwa ni kukuza kilimo na kuongeza mavuno ya mazao ambayo ndio malighafi kuu inayohitajika wakati huu ambapo serikali inatekeleza mipango ya ukuaji wa viwanda, kama msingi mkuu wa kufikia malengo ya kuwa taifa la uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
No comments