Breaking News

Taarifa muhimu ya TCU kwa wanafunzi waliokosa vyuo


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa awamu ya kwanza ya Udahili wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali ulimalizika tarehe 30 Agosti 2017. Tume inawaarifu kuwa imekamilisha zoezi la uhakiki wa majina ya waombaji wote walioomba kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo wa 2017/18. Hata hivyo kutokana na waombaji wengi kutochaguliwa kutokana na sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 4 hadi 10 Octoba 2017 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili: • Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza; • Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanza; • Waombaji wenye vigezo vya Stashahada walioshindwa kupata Namba ya Uhakiki wa Tuzo (AVN); • Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2017 na matokeo yao yameshatoka; na • Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitsho toka vyuo vyao vya awali. Aidha Tume inapenda kusisitiza kuwa utaritibu wa kutuma maombi ni ule ule uliotumika katika awamu ya kwanza ya Udahili. Imetolewa na Prof. Eleuther Mwageni Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania 4 Oktoba 2017

No comments