Zitto Kabwe Alia na Kibano Kipya Vyama vya Siasa
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa serikali ya awamu ya tano inadhamira ya kuuwa vyama vya upinzani nchini kwa muswada wa sheria ambao umesambazwa kwenye vyama vya siasa.
Zitto Kabwe anasema muswada huo ambao umesambazwa tayari kwa vyama vya siasa ni kama hukumu ya kuviuwa vyama vya upinzania nchini kwani kuna vifungu ambavyo vinakataza vyama vya siasa kisheria kufanya mikutano ya hadhara isipokuwa mwaka wa uchaguzi tu, lakini pia watu wanaoruhusiwa kufanya mikutano hiyo ni wabunge na madiwani tu kwenye majimbo yao husika.
Kufuatia jambo hilo Zitto Kabwe amesema kuwa hawatakubali jambo hilo na watapinga sheria hiyo ndani ya Bunge pamoja na nje ya bunge na kusema wao watalinda mfumo wa vyama vingi nchini kwa gharama yoyote kwani uwepo wa vyama ni haki Kikatiba.
No comments