Breaking News

Aliyetangazwa kununua nyumba za Lugumi akamatwa na Polisi


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Dk. Luis Shika ambaye mapema leo alitangazwa kununua nyumba mbili za Lugumi zilizokuwa zikipigwa mnada na Kampuni ya Udalali ya Yono (Yono Auction Mart).

Taarifa iliyotokana na mnada huo mapema leo mchana zilieleza kuwa Dk Shika amenunua nyumba hizo mbili zilizopo eneo la Mbweni, Dar es Salaam kwa gharama ya Tsh 1.9 bilioni.

Taarifa kutoka Yono zinaeleza kuwa, mnada wa nyumba hiyo unarudiwa tena leo baada ya kubainika kuwa Dk Shika ni tapeli na kwamba ameshindwa kulipia fedha asilimia 25 kama masharti ya mnada huo yanavyotaka.

Akiwajibu waandishi wa habari maswali yao, Dk Shika alisema kwamba, Yono walitaka 25% ya fedha za nyumba hizo, ambapo yeye hakuwa na kiasi hicho cha fedha kwa wakati huo.

Aidha, alifafanua kwamba, kiasi hicho cha fedha kingeweza kupatikana kesho au keshokutwa kwa sababu huwa hatembei na fedha kamili mfukoni.

No comments