Waziri Mwakyembe Awapa Pole Clouds Media Group Baada Ya Ofisi Zao Kupata Ajali Ya Moto
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amepokea kwa mshtuko na masikitiko taarifa za ajali ya moto kwenye ofisi za kituo cha Redio na Televisheni cha Clouds Media cha Jijini Dar es Salaam hapo jana.
Waziri huyo ambaye yuko mkoani Iringa kwa ziara fupi ya kikazi, ametoa pole kwa viongozi na wafanyakazi wa kituo hicho cha redio na televisheni kwa kuunguliwa na baadhi ya vifaa vya kazi vya chombo hicho cha habari na kuzitaka Taasisi husika kufanya uchunguzi wa kina kujua chanzo cha moto huo.
Aidha, Dkt. Mwakyembe amelipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini kwa kuitikia wito na kufika kwa haraka sehemu husika na hivyo kudhibiti moto huo usilete madhara makubwa zaidi.
Imetolewa na:
Lorietha Laurence
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
22/11/2017.
No comments