Wema Sepetu: Sina Mpango wa Kurudi CCM
Mrembo wa Tanzania na Muigizaji Wema Sepetu amemfunga mdomo muigizaji mwenzake Steve Nyerere kwa kumwambia hana mawazo ya kurudi CCM kama jinsi ambavyo wengine wanavyofanya.
Wema amefanya tendo hilo kwa kujibu ujumbe wa Steve Nyerere aliokuwa ameuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram akimkaribisha ndani ya CCM, Wakili Alberto Msando ambaye mapema jana alitangaza kujiunga na CCM.
Steve aliandika "Sasa utakuwa mzalendo wa kweli , Msando naheshimu maamuzi yako maana ni maamuzi sahihi, kwako pamoja na family yako , rafiki zako nasi tupo pamoja nawe, soon na yuleeeeeeeee rafiki yetu , dada yetu , msanii mwenzetu , naye yupo njiani kurudi nyumbani"
Hata hivyo Wema Sepepetu baada ya kuona ujumbe huo ambao alihisi kama inamlenga yeye, alijibu chini ya ujumbe huo kwa kuandika "I hope hauniongelei mimi... Maana mawazo hayo sina"
Muigizaji Wema Sepetu alihama ndani ya chama cha mapinduzi Februari mwaka huu kwa madai kuwa ameamua kujiunga na Chadema kupigania demokrasia ya kweli.
No comments