Breaking News

Godbless Lema Afichua Wanachohongwa Wabunge wa CHADEMA Ili Wahamie CCM


Mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema amefunguka na kusema ahadi ambazo baadhi ya viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakipewa jambo linalopelekea kujiuzulu na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Lema amesema hayo jana Disemba 14, 2017 mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Ole Mollel kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na uanachama wa CHADEMA kuanzia jana  na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Nitakupa mshahara wako wote kwa miaka iliyobaki, pia nitakulipia madeni yako yote, nitakupa kiinua mgongo chako chote nitakupa na mlinzi kwa kipindi hiki na ukitaka tena kugombea nitakupa kipaumbele wewe au kazi nyingine utakayotaka? Je, utakuwa tayari? Si utakuwa tiyari wajameni?" aliandika Lema kwenye mtandao wake wa Twitter

Baadhi ya vyama vya upinzani nchini vimekuwa vikikumbana na changamoto ya baadhi ya viongozi wao au wananchama kujivua uanachama na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile wanachodai wanaunga mkono juhudi na utendaji kazi wa Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli.

No comments