Breaking News

Godbless Lema, Jerry Muro Wazidisha Utata Safari Ya Mnyika Kuhamia CCM


Licha ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kukaririw jana kikikanusha fununu zilizozagaa mitandaoni zikielekeza kuwa Mbunge wa Kibamba (Chadema), Mhe. John Mnyika anatazamiwa kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM), bado ishara zimezidi kuonesha kuwa safari ya kinara huyo wa upinzani kuelekea CCM imezidi kuiva.

Tetesi hizo zimegonga vichwa vya mitandao ya kijamii jana jioni  baada ya kada wa CCM, Jerry Muro kutumia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuweka picha ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli na John Mnyika na kuandika maneno kadhaa kama ifuatavyo;

“Wanakuita mvulana, basi nenda kwa Baba ukadeke kidogo kule ulikua unakomazwa tu, #safarimojamatata.”
Wakati wengi wakitafakari maneno ya Jerry Muro, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) naye ametumia mtandao wa kijamii kuandika machache yaliyotafsiriwa kama maneno yanayoongelea sakata la Mnyika kutimkia CCM. 

==>Lema ameandika yafuatayo;

No comments