Breaking News

Hakuna Mapenzi Tena Kati ya RayVanny na Fahyma ?

Mwimbaji Staa wa Bongo fleva RayVanny usiku wa December 12 kuingia 13 alipost ujumbe kupitia ukurasa wake wa instagram unaoashiria kuwa kuna tatizo kati yake na mpenzi wake Fahyma hiyo ni baada ya kupost picha yake ikiwa na caption tata.

Rayvanny aliandika hivi “mpende ila usimuamini, mpe ila sio vyote, mtunze ila usimchunge, mpe mwili wako ila usimpe siri zako hata mkojo ulikuwa soda, vitamu ndio vichungu keep it your mind”

Kutokana na kile ambacho Rayvanny alikipost kupitia mtandao huo wa instagram ulizua maswali mengi kwa baadhi ya mashabiki na wengi kujiuliza kama ni kiki au ni kweli maana Fahyma nae alipost picha yake na kuandika “single mama” AyoTV na millardayo.com zinamtafuta Rayvanny azungumzie ishu hiyo.

No comments