Breaking News

Mnyika aungana na Rais Magufuli


Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, katika kuomboleza vifo vya askari 14 waliouawa nchini Kongo na wengine kujeruhiwa, huku akiwapa pole wafiwa wote.

Mbunge wa Kibamba ameitumia Jumapili ya leo Disemba 10,2017  kuwaombea mashujaa hao na kuwapa pole wanafamilia wote ambao ndugu zao wamepoteza maisha katika tukio hilo.

"Kwa kipekee naitoa ibada ya leo kuwaombea Mashujaa wetu,askari 14 wa JWTZ waliojitoa mhanga na maisha yao kuitetea amani Congo, 44 ambao wamejeruhiwa na wale wawili (2) ambao hawajulikani walipo. Mungu awajalie pumziko jema kwa wale waliopoteza uhai kupigania amani

"Awape uponyaji majeruhi na kusaidia kupatikana kwa Askari wawili. Aijalie faraja na ustawi familia za wahanga na wote ambao wameguswa kwa moja kwa moja au namna ingine yeyote na tukio baya hilo" aliandika John Mnyika

No comments