BREAKING: Rais Magufuli ametangaza Ruge Mutahaba amefariki
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa masikito makubwa, kupitia ukurasa wake rasmi twitter Rais Magufuli ametangaza kuwa Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba amefariki dunia.
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kijana wangu Ruge Mutahaba. Daima nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk tasnia ya habari, burudani, na juhudi za kujenga fikra za maendeleo kwa vijana. Poleni wanafamilia,ndugu,jamaa na marafiki. Mungu amweke mahali pema, Amina”
Ruge Mutahaba hadi umauti unamkuta alikuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini, Ruge amekuwa akiugua kwa zaidi ya miezi minne na alianza kupatiwa matibabu Dar es salaam, India na baadae Afrika Kusini, millardayo.com imezipokea taarifa za msiba wa Ruge kwa masikitiko makubwa, siku zote utakumbukwa mchango wa Ruge katika tasnia ya habari na burudani, pumzika kwa amani Ruge.
No comments