Mrembo amesoma Masters Marekani ila anauza makande Mwanza (+video)
Nancy Lema ni msomi wa Elimu ya Masters ya Project Management Chuo cha SAINT MARY’S UNIVERSITY OF MINNESOTA Nchini Marekani na ameishi Marekani kwa miaka 10, mwaka 2015 aliamua kurudi rasmi Tanzania na kwenda kwao Mwanza na kuanza kutafuta kazi kwenye Makampuni bila mafanikio ndipo akaja na wazo la kuuza chakula aina ya makande kwenye ofisi Mwanza.
“Nilijua nimemaliza Masters yangu nakuja Tanzania kutafuta Kazi haitakuwa ngumu lakini kila sehemu niki-apply naambiwa subiri kwanza ilinifanya nifikirie nini cha kufanya” Nancy Lema
” Wazazi wangu hawakukubliana na mimi nianze kupika wakati wamenisomesha walitegemea niwe Meneja Kampuni flani na elimu kubwa, Ila kwa sasa ndio Wateja wangu wakubwa” Nancy Lema
No comments