Taarifa Ya Ajali Ya Gari Kuungua Moto Na Kusababisha Majeruhi Na Uharibifu Wa Mali Mkoani Mbeya.
Mnamo tarehe 02.01.2020 majira ya saa 16:05 jioni huko eneo la Meta-Igurusi katika barabara kuu ya Mbeya/Njombe,
Gari lenye namba za usajili T. 956 DRT/T. 886 DRV aina ya Scania Tanker la Mafuta mali ya kampuni ya “world oil” lililokuwa limepakia mafuta aina ya Petroli kutokea Dar es salaam kuelekea nchini Zambia likiendeshwa na dereva ISSA YUSUPH [35] mkazi wa Jijini Dar es Salaam lilipata hitilafu za kiufundi siku ya tarehe 01/01/2020 majira ya saa 16:30 jioni na baadae liliungua moto na kuteketea wakati wa harakati za kufaulisha mafuta kwenye gari hiyo kwenda kwenye gari namba T 844 AWJ Trailer na kusababisha majeraha kwa watu wawili.
Watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo ya moto ni:-
1. JULIUS DAUDI [30]
2. STANFORD MWAKYUSA [45]
wote wakazi wa Igurusi Wilayani mbarali.
Aidha katika ajali hiyo kulitokea uharibifu kwa gari namba SM 4633 aina ya Isuzu mali ya Jeshi la Zimamota na Uokoaji na gari namba T 844 AWJ Trailer.
Chanzo cha ajali ni mlipuko uliotokea kwenye mashine ya kufaulishia mafuta aina ya “water pump”. Majeruhi wamekimbizwa kituo cha afya igurusi kwa matibabu.
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments