Breaking News

Urusi yakana kuwashambulia wapiganaji wanaoungwa mkono na Marekani nchini Syria

 A Su-24 bomber takes off from the an airbase in Syria (file picture)

Wizara ya ulinzi nchini Urusi imekana madai kuwa ndege zake zilishambulia wapiganaji wanaoungwa mkono na Marekani nchini Syria siku ya Jumapili.
Wizara hiyo ilisema kuwa jeshi lake la wanahewa lililenga wapiganaji wa Islamic State.
Jeshi la Urusi lilikuwa likijibu madai ya SDF ambao ni muungano wa wakurdi na makundi ya kiarabu kuwa wapiganaai wake sita walijeruhiwa kwenye mashambulizi ya angani ya Urusi mashariki mwa Syria.

Pro-Syrian government militiamen sit in the back of an armed vehicle in Bir Qabaqib, west of Deir al-Zour (4 September 2017) 
 
SDF wanasonga mbele kuelekea mji wa Deir al-Zour ambapo vikosi vinavyoiunga mkono serikali , vinavyosaidiwa na Urusi, vinataka kuuteka mji huo kutoka kwa IS.
Siku ya Jumamosi Syrian Democratic Forces (SDF), walisema kuwa saa za asubuhi siku hiyo, wapiganaji wao mashariki mwa mto Euphrates walilengwa na ndege za Urusi pamoja na za Syria.
Lakini leo Jumapili msemaji wa wizara ya ulinzi ya Urusi meja jenerali Igor Konashenkov, alisema kuwa ndege za Urusi ziliwalenga wapiganaji wa IS katika mkoa wa Deir al-Zour.
Syrian army officers and pro-government militiamen inspect the desert from Bir Qabaqib, west of Deir al-Zour (4 September 2017)























No comments