Watano Watiwa Mbaroni kwa Kumuombea Tundu Lissu
Jeshi
la Polisi jijini Dar es salaam, linawashikilia watu watano kwa tuhuma
za kuratibu shughuli za maombezi maalum kwa ajili ya mbunge Tundu Lissu,
katika viwanja vya TIP Sinza.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni Murilo
Jumanne aliyekuwa eneo la tukio, amesema wameamua kuwakamata watu hao
kwa kuwa wanatishia amani na utulivu wa nchi.
"Wale
wenye nia mbaya ambao bila shaka wana ajenda binafsi ajenda ambazo
kimsingi zina uelekeo wa kutishia masuala ya amani, mimi kama Kamnda wa
Polisi mkoa wa Kinondoni, siwezi kukubali hali hiyo itokee kwenye eneo
langu, watu wanaendelea na shughuli zao na wachache wakiwa wamevaa nguo
za kawaida lakini wameficha tishirt ndani, wanafika sehemu wanaanza
kuzitoa", amesema Kamanda Jumanne.
Kamanda
Jumanne ameendelea kwa kuwataka wananchi kuacha kufanya mikusanyiko ya
aina hiyo, na iwapo wanahitaji kufanya ibada waende kwenye sehemu za
ibada.
Jana
Jeshi la polisi Kanda maalum lilitoa taarifa ya kupiga marufuku
kusanyiko lolote lisilo halali kumuombea Mbunge Tundu Lissu ambaye yuko
Nairobi kwa matibabu, na kusema ni kuhatarisha hali ya amani.
No comments