Breaking News

Watu 14 watiwa mbaroni kwa kupinga mabadiliko ya ukomo wa umri wa rais


Watu 14 wametiwa mbaroni katika mji mkuu wa Uganda kampala kufuatia maandamano ya kupinga mapendekezo ya muswada wa sheria unaoondoa kikomo cha umri wa mtu anayegombea urais. Katiba ya sasa ya Uganda inasema kuwa kikomo cha mtu kugombea kiti cha urais ni umri wa miaka 75. hivyo mabadiliko yeyote ya katiba yatakayofanywa yatamruhusu Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni kugombea tena urais mwaka 2021. Aidha, Umri halisi wa Rais Yoweri Museveni haufahamiki ingawa mitandao mbalimbali ya kijamii imeandika kuwa rais huyo ana umri wa miaka 73 kitu ambacho hakijathibitishwa na mtu yeyote kuhusu ukweli wa umri huo. Hata hivyo, Wanaharakati vijana wa kundi lijulikanalo kama-The Alternative, ambao waliandaa maandamano ya kupinga muswada huo wa mabadiliko ya katiba wamesema kuwa ofisi yao ilivamiwa na Askari polisi na kunyang’anywa kompyuta na nyaraka mbalimbali.

No comments