Baada ya malezi Linah kurejea na Recho
Msanii wa muziki Bongo Linah amefunguka ujio wake mpya baada ya kujifungua.
Muimbaji huyo amesema baada ya mtoto wake kufikisha miezi mitano anaona ni wakati mzuri wa kurejea katika game.
“Mtegemee wimbo mpya mwezi huu wa 12 mwishoni nimefanya collaboration na Recho wa Kizunguzungu, nafikiri wiki ijayo tutaachia” Linah ameiambia Bongo5.
Kufanya kwa kolabo hiyo itakuwa ni mara ya pili kwa Linah na Recho kukutana katika ngoma moja baada ya kushirikishwa na kundi la Makomando katika ngoma yao inayokwenda kwa jina la Chap Chap.
No comments