Gabo adai Bongo Movie wanafanya kazi zisizo zao
Msanii wa Filamu Bongo, Gabo amesema wasanii wengi wa filamu nchini wanafanya kazi ambao haziwahusu.
Muigizaji huyo akizungumza na E-Newz ya EATV amesema kitu hicho kimefanya tasnia hiyo kushuka kwa mwaka huu na kinachotakiwa sasa ni wafikirie namna ya kujifunza.
“Unapoacha kazi yako ukafanya kazi ya mwenzako ina maana unaharibu ya kwako, kazi ambazo zilikuwa zinafanywa na wengi katika wao ambao walikuwa wanafanya kazi ambazo si za kwao, unajua hata ukiwa si mwanachuo ukaenda kuzindua majengo ya chuo unaweza ukawachanganya wakashindwa kufahamu wewe taaluma yako ipo wapi,” amesema Gabo.
Kauli ya Gabo inakuja mara baada ya kuonekana wasanii wengi wa Bongo Movie kujiingiza zaidi katika siasa. Utakumbuka hivi karibuni muigizaji Aunt Ezekiel alinukuliwa akisema wasanii wa movie wanaofanya hivyo kutokana wamekosa kazi za kufanya.
No comments