Barakah The Prince azidi kulia mchezo mchafu YouTube
Msanii wa muziki Bongo, Barakah The Prince amedai kuwa bado video zake zinafanyiwa hujuma katika mtandao wa YouTube.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Sometimes’ ameiambia XXL ya Clouds Fm hata ngoma yake mpya imefanyiwa hivyo ila vigumu kuwatambua wanaofanya hivyo
“Hiyo ishu ilianzia kwenye video yangu ya Sometimes views hawapandi, subscriber wanasimama, likes wanashuka, dislike wanakuwa ni wengi, wimbo unafanya vizuri mtaani halafu dislike zinakuwa ni nyingi, kwa hiyo kuna mchezo nilikuwa nafanyiwa ambao ni the same kwenye Nipe Nguvu,” amesema Barakah.
“Na promotion yote ninayokuwa naifanya kwenye mitandao ya kijamii views wanakuwa hawapandi, kuna wasanii ambao ni underground ambao sidhani kama wana mashabiki kama vile ninao mimi tumetoa video pamoja lakini views zao zinapanda kitu ambacho si cha kawaida,” ameongeza.
No comments