Breaking News

Mwaka 2018 utakuwa nzuri zaidi kwa Bongo Movie – JB

Msanii mkongwe wa filamu Jacob Stephan aka JB amefunguka kwa kuitabiria tasnia ya Bongo Movie kufanya vizuri zaidi mwaka 2018 kutokana na maandalizi mazuri yaliyofanywa mwaka 2017.


Muigizaji huyo amedai wasanii wengi awamefanya maandalizi makubwa katika kufungua kampuni za kusambaza filamu pamoja na kuzipeleka filamu kwenye majumba ya sinema.
“Mwaka 2018 itakuwa nzuri zaidi kwa BongoMovie kwani ukiangalia kurasa zao tayari wamerudi kwenye kazi zao. Kitu ambacho tulikuwa tukitamani ni ujio wa makampuni ya usambazaji, barazani, max burudani umeongeza chachu zaidi kwani hilo lilikuwa tatizo kubwa,” aliandika JB kupitia Instagram.
Aliongeza, “Lakini pia kumekuwa na utengenezaji wa tamthilia nyingi ambazo zitashindana sana mwezi January. Uzinduzi wa filamu mbalimbali kwenye kumbi kubwa tena zikionyeshwa live kwenye TV nalo limekuwa jambo zuri. Nawapongeza waandaji wote wanao hakikisha Bongo Movie inashika kasi mpya, hongereni.
Muigizaji huyo mwanzoni mwa mwaka 2017 alisema ifikapo mwisho wa mwaka 2018 atatangaza kustaafu kuigiza na kubaki kama producer tu.

No comments