EXCLUSIVE: Vanessa Mdee afunguka jinsi alivyopata dili la Universal Music Group (+Video)
Msanii wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amefunguka kwa mara ya kwanza jinsi alivyopata dili nono na Kampuni kubwa ya usimamizi wa kazi za wasanii wakubwa duniani ya Universal Music Group.
Vanessa Mdee amesema hakutarajia chochote kuhusu dili hilo bali ni hao wenyewe UMG waliokuwa wakifuatilia kazi zake na hatimaye kutamani kufanya kazi naye.
Kuhusu kiasi gani atalipwa kwenye dili hilo ambalo yeye mwenyewe amekiri kuwa ni msanii wa kwanza wa kike barani Afrika kusaini dili kama hilo lenye thamani ya mamilioni ya pesa, Vee Money amefunguka zaidi kwenye mahojiano yake na Bongo5 msikilize hapa chini
No comments