Lulu Diva Kufunga Ndoa Ya Kimya Kimya
Mrembo anayefanya poa Bongo Flevani, Lulu Abas ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa japokuwa ndoa yake imekaribia lakini hahitaji kelele kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza na gazeti hili, Lulu Diva alisema anamshukuru Mungu mipango yake ya harusi inaenda sawa, lakini ameamua kufanya kimyakimya kwa sababu hapendi iwe gumzo.
“Yaani ndoa yangu sitaki kabisa vurugu mbalimbali watu watasikia tu tayari nimeolewa, nashukuru Kila kitu kimeenda sawa katika maandalizi, baadhi ya watu nitakaowachagua kuhudhulia watapata mualiko tu,” alisema
No comments