Mtoto wa mwaka 1 afukiwa kichwa chini kiwiliwili juu (+video)
Jeshi la Polisi mkoani, linawashikilia watu wawili ambao ni Mume na Mkewe wakazi wa Mtaa wa Pambogo katika Kata ya Iyela jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wao wa kumzaa kisha kumfukia.
Akizungumza na wandishi wa habari ofsini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei amesema tukio hilo lilitokea Disemba 22 mwaka huu saa 12:30 alfajiri.
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Ally Mbavu (23) na Sabina Alex (19) ambao wanadaiwa kusababisha kifo cha mtoto wao wa kiume, Ismail Mbavu (mwaka mmoja na miezi 11).
No comments