Watu wanne wameua tembo wanne “Hii si dili Milioni 137 bei yake” (+video)
Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya baada ya kukamatwa wakiwa na vipande 11 vya meno ya tembo yenye uzito wa KG 21 ambayo yanadaiwa kuwa na thamani ya zaidi ya Milioni 137.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Ulrich Matei amesema watuhumiwa wamekamatwa wakiwa maeneo ya Soweto Jijini baada ya kuwekewa mtego na Jeshi la Polisi ikiwa ni baada ya kupata taarifa kuwa meno hayo ya tembo yamesafirishwa kutoka Mkoani Njombe na kuingizwa jijini Mbeya.
No comments