Jafo akabidhi Mashine 7227 Za Kukusanyia Mapato Ya Kielektroniki
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa[TAMISEMI] Mhe.Seleman Jafo amekabidhi mashine elfu saba ,mia mbili na ishirini na saba[7227] za kukusanyia mapato ya kielektroniki [PoS] kwa serikali za mitaa huku akitoa kiama kwa halmashauri ambazo zitafanya uzembe katika ukusanyaji wa mapato hayo.
Akizungumza jana Januari ,22,2020 jijini Dodoma mbele ya wakurugenzi wa halmashauri,makatibu tawala wa mikoa ,Waziri Jafo amesema mashine hizo itakuwa ukombozi mkubwa wa ukusanyaji mapato na kuagiza Wakurugenzi kukusanya mapato vyema na haitakuwa kisingizio tena juu ya ukusanyaji mapato hayo.
Aidha,Waziri Jafo amesema pamekuwepo na suala la Wakusanya mapato Wasiokuwa waaminifu kwa baadhi ya halmashauri hivyo uwepo wa Mashine hizo itaongeza chachu ya Uwazi wa ukusanyaji mapato huku akiishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa kusaidia Mashine hizo za PoS kwa kushirikiana na Serikali ya Norway.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo ametoa rai kwa halmashauri ambazo hazijalipa madeni ya Madiwani kulipa mara moja kwani hadi sasa halmashauri kubwa inadaiwa Milioni 758.
No comments