Kauli Kangi Lugola Baada ya Rais Magufuli Kumtumbua na Kusema Hafai
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema ataendelea kumsaidia Rais Magufuli kwa kuwa yeye ni mbunge wa Mwibara (CCM).
Lugola ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Januari 23, 2020 jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya uzinduzi wa nyumba za maofisa wa Jeshi la Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Alieleza hayo baada ya Rais Magufuli ambaye wakati akizungumza katika uzinduzi huo kusema Lugola na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye hawafai kuendelea na nyadhifa zao kutokana na mambo waliyoyafanya kuhusu uingiaji wa mikataba.
“Rais ndiye aliniteua kwenye Baraza la Mawaziri na ndiye ameona anipumzishe, kwangu mimi ni jambo la faraja, Watanzania mmemsikia Rais hatua aliyochukua ni hatua nzuri na inalenga kujenga safu ya Serikali, ninaahidi kama Mbunge ambaye nilipata nafasi ya kumsaidia Rais nitaendelea kumsadia kwa kwa heshima kubwa." Amesema Lugola

No comments