Breaking News

Mauaji ya Kamanda wa Jeshi la Iran: Marekani Yawataka Raia Wake Kuondoka Iraq Haraka....Jeshi la Israel Lawekwa Katika Hali ya Tahadhari Kubwa

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahuu ameikatiza ziara yake ya Ugiriki kufuatia kuuawa kwa Meja Jenerali Qassem Soleimani, mkuu wa jeshi maalum la Iran. 

Hayo ni kwa mujibu wa afisa mmoja kutoka ofisi ya Waziri Mkuu huyo. 

Netanyahu amekuwa mjini Athens kufuatia muafaka uliotiwa saini na Ugiriki, Cyprus na Israel hapo jana, wa kujenga bomba la kusafirisha gesi asili kutoka eneo linakopatikana mafuta la mashariki ya Mediterania hadi Ulaya.

 Redio ya Jeshi la Israel imeripoti kuwa jeshi la nchi hiyo liko katika hali ya tahadhari kubwa, likihofia ulipizaji kisasi wa Iran au washirika wake baada ya kuuliwa kwa Soleimani katika shambulizi la angani mjini Baghdad. 

Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani imewataka raia wa Marekani kuondoka nchini Iraq haraka iwezekanavyo. 

Shughuli za ubalozi wa Marekani mjini Baghdad zilisitishwa mapema wiki hii kufuatia mashambulizi kwenye jengo la ubalozi na wafuasi wa wanamgambo wanaoungwa mkono na Ir

No comments