Breaking News

Penzi la Rihanna na Bilionea wa Kiarabu Lavunjika

Taarifa za watu wa karibu na msanii Rihanna zinaeleza kuwa penzi lake na bilionea wa kiarabu Hassan Jameel, limefikia ukomo baada ya kudumu kwenye mahusiano kwa muda wa miaka mitatu.

Kwa mujibu wa taarifa ya mitandao mbalimbali Duniani, Rihanna na Jameel walianza uhusiano wao wa kimapenzi mwaka 2017 lakini ulikuwa uhusiano wa faragha. Bado haijabainika wazi chanzo cha wawili hao wenye umri wa miaka 31 kuamua kutengana. 

Jameels wanaorodheshwa wa 12 kama familia tajiri miongoni mwa Waarabu kulingana na jarida la Forbes. 

Habari za wawili hao kuchumbiana ziligonga vichwa vya habari baada ya kupigwa picha wakifanya yao  katika kidimbwi cha kuogelea nchini Uhispania. 

No comments