Mrema azungumzia uamuzi wa Rais Magufuli Kusamehe Wafungwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema amepongeza uamuzi wa Rais John Magufuli wa kutoa msamaha kwa wafungwa na kumuelezea kama Rais mwenye upendo wa aina yake.
Mrema amesema ni wazi kuwa Rais amesikia kilio cha watu na kuamua kufanya ubinadamu ili kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani.
“Namvulia kofia kabisa, huyu ni Rais msikivu, ana mapenzi ya kweli kwa Watanzania naweza kusema tumepata mtu ambaye tulikuwa tunamtaka,”
Mrema amesema upo uwezekano kuwa Rais alikuwa hapewi taarifa sahihi kuhusu hali ya magereza.
“Magerezani kuna uozo, wapo watu wengine wanajaa kule kwa makosa ambayo wanaweza kulipa faini tu wakatoka,”
“Nilianzisha kampeni ya kuwalipia faini wafungwa ambao walishindwa kujilipia lakini kutokana na maslahi ya baadhi ya watu nikaambiwa nisitishe kwa madai kuwa wafungwa hao hawajajutia makosa. Hii si sawa, naomba watu wa magereza wabadilike hakuna sababu ya kuwajaza wafungwa kule ambao wanatakiwa kutoka,”
No comments